Bomu hilo lililipuka ndani ya soko la Macampagne katika mji wa Beni, ambako watu 17 walijeruhiwa na kupelekwa kwenye vituo vya matibabu, amesema Tharcisse Katembo, mkuu wa wilaya huko Beni.
Mwandishi wa AFP aliona watu wanane waliojeruhiwa, wakiwemo wasichana watatu, wakihudumiwa kwenye hospitali.
Waathirika walipata majeraha kwenye miguu, mikono na kichwani, mwandishi huyo amesema.
“Kijana mmoja aliacha mfuko wa plastiki wa rangi ya kijani kibichi, akiahidi kurejea kuuchukua. Dakika tatu baadaye, mfuko huo ulilipuka na kuwajeruhi watu na mimi nikiwemo na wateja waliokuja kusaga mihogo,” Dany Siauswa, meneja wa kiwanda hicho cha kusaga, ameiambia AFP.
Facebook Forum