Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 10:19

Bomu la Kwenye Gari Lauwa Watu 50 Nchini Libya


Wapiganaji wanaonekana wakilenga silaha kwenye viunga vya Sidra, Libya Desemba 14, 2014.
Wapiganaji wanaonekana wakilenga silaha kwenye viunga vya Sidra, Libya Desemba 14, 2014.

Bomu la kwenye gari magharibi mwa Libya limeuwa karibu watu 50 na kujeruhi wengine kadhaa katika kituo cha mafunzo ya polisi kwa mujibu maafisa wa polisi na ripoti za mjini humo.

Bomu hilo lilipuka wakati mamia ya wanafunzi hao wa polisi wakiwa wamekusanyika katika eneo la mji wa Zliten. Duru zinaeleza watu wasiopungua 50 waliuwawa chanzo cha habari cha hospitali kimelieleza shirika la habari la Reuters idadi ya waliofariki imefikia 65.

Hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi hilo.

Kwenye mtandao wa Twitter mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa kwa Libya (UNSMIL) amesema bomu hilo ni kama shambulizi la kujitoa mhanga.

XS
SM
MD
LG