Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:05

Bomu ndani ya gari limeuwa watu watatu Somalia

Polisi wa somalia wakiangalia gari lililoharibiwa na bomu ndani ya gari
Polisi wa somalia wakiangalia gari lililoharibiwa na bomu ndani ya gari

Kamishna wa polisi Mogadishu, Ali Hersi Barre, amesema dereva wa gari hilo aliyekamatwa amejeruhiwa vibaya kutokana na mlipuko huo.

Polisi wa Somalia wanasema mlipuko wa bomu moja lililotegwa ndani ya gari nje ya duka linalouza chai karibu na jengo la polisi mjini Mogadishu hii leo limeuwa maafisa wasiopungua watatu.

Kamishna wa polisi Mogadishu, Ali Hersi Barre, amesema dereva wa gari hilo aliyekamatwa amejeruhiwa vibaya kutokana na mlipuko huo.

Barre amesema polisi wanachunguza tukio hilo.

Shambulizi la leo linafuatia shambulizi moja lililofanyika jumatatu katika mji wa Beledweyne, ambako watu wasiopungua sita wakiwemo wanajeshi wawili wa Umoja wa Afrika walijeruhiwa katika mlipuko kwenye uwanja wa ndege.

XS
SM
MD
LG