Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 06:29

Boko Haram yafanya uharibifu zaidi katika mashambulizi yake


Kundi la wanamgambo wa Boko Haram la nchini Nigeria
Kundi la wanamgambo wa Boko Haram la nchini Nigeria

Kundi moja la haki za binadamu limetoa picha za satelaiti ikielezewa zinaonyesha uharibifu huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria uliofanywa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.

Amnesty International inasema picha za kabla na baada kwenye eneo la Baga na eneo jirani la Doron Baga zinaonesha kuwa majengo takriban 3,700 yalichomwa hivi karibuni baada ya kundi la Boko Haram kuchukua udhibiti wa Baga hapo Januari 3 mwaka huu. Uharibifu mkubwa wa nyumba ulikuwa huko Doron Baga ambako mtafiti wa Amnesty, Daniel Eyre alisema umeharibi kabisa ramani ya mji katika muda wa siku nne.

Kundi la kutetea haki za binadamu, Amnesty International
Kundi la kutetea haki za binadamu, Amnesty International

Pia kundi hilo la haki za binadamu lilisema mahojiano na mashahidi pamoja na maafisa katika eneo yanapendekeza kuwa wanamgambo wamewafyatulia risasi mamia ya raia wakiwemo watoto wadogo na mwanamke mmoja ambaye alikuwa anataka kujifungua.

Jeshi la Nigeria liliweka idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Baga kufikia 150, lakini maafisa wa eneo walisema huwenda ikawa zaidi ya 1,000. Amnesty International ilisema jumatano kuwa kulingana na utafiti wao kundi la Boko Haram huwenda lilishambulia Baga kwa sababu ilikuwa makazi ya kikosi maalum cha Civilian Joint Task force, kundi la watu wanaolisaidia jeshi kupambana na wanamgambo wa kiislam.

Awali jeshi la Nijeria lilisema lilizima shambulizi la Boko Haram kwingineko katika jimbo la Borno. Jeshi lilisema kwenye mtandao wake wa Twitter kwamba wanajeshi walirudisha nyuma “shambulizi la ugaidi” mapema jumatano kwenye mji wa Biu. Linasema wanajeshi walikuwa wakiwasaka washambuliaji baada ya kuwakamata watu watano wenye silaha na zana nyingine.

XS
SM
MD
LG