Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 12:51

Boko Haram wauwa mamia zaidi Nigeria


Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau anakiri kuwa kundi lake lilihusika na utekaji wa wasichana wanafunzi takribani 300
Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau anakiri kuwa kundi lake lilihusika na utekaji wa wasichana wanafunzi takribani 300
Mamia ya watu wanakhofiwa kufa baada ya wanamgambo kushambulia mji mmoja huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria na kuchoma moto nyumba na biashara na kuwafyatulia risasi wakazi wakati wakijaribu kukimbia.

Maafisa wa eneo wanasema washukiwa wanamgambo wa Boko Haram walishambulia mji mmoja wa ndani wa Gamboru Ngala, unaopakana na Cameroon. Ripoti za habari zinasema zaidi ya nyumba 250, soko kubwa sana katika mji huo na kituo kimoja cha polisi viliharibiwa.

Wakati huo huo, jeshi la Marekani linatoa maelezo kuhusu timu moja ya wataalamu wanaoelekea Nigeria kusaidia kuwatafuta wasichana wanafunzi 276 waliotekwa na kundi la Boko Haram. Msemaji wa Pentagon, kanali Steve Warren anasema timu hiyo itawasili katika siku chache zijazo.

Warren anasema Marekani haifikirii kufanya operesheni za kijeshi katika juhudi za kuwaokoa wasichana hao.
XS
SM
MD
LG