Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:29

Boko Haram watishia kuvuruga uchaguzi mkuu Nigeria


Kundi la wanamgambo wa Boko Haram la nchini Nigeria
Kundi la wanamgambo wa Boko Haram la nchini Nigeria

Mkuu wa kundi la kigaidi la Boko Haram la nchini Nigeria ametishia kuvuruga uchaguzi wa nchi hiyo ambao tayari umeahirishwa mpaka mwezi ujao kwa sababu ya khofu ya ghasia.

Katika kanda mpya ya video iliyobandikwa kwenye mtandao jumanne, mkuu wa kundi la Boko Haram, Abubakar Shekau alisema hata kama mapigano yatasababisha vifo kwa wapiganaji wake, mungu hataruhusu uchaguzi huo uendelee.

Kundi hilo mara kwa mara lilionya wa-Nigeria kutojitokeza katika upigaji kura ambao sasa umepangwa kufanyika Machi 28. Uchaguzi awali ulipangwa kufanyika Februari 14 mwaka huu. Mabomu yalilipuka katika sehemu tatu tofauti nchini Nigeria jumanne na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Wanamgambo wa Boko Haram
Wanamgambo wa Boko Haram

Ghasia hizo ni pamoja na shambulizi katika mkutano wa hadhara wa chama cha upinzani cha APC katika mji wa Okrika uliopo katika jimbo la kusini la Rivers. Chama cha APC kilileta upinzani mkali dhidi ya chama tawala cha PDP cha Rais Goodluck Jonathan ambaye analaumiwa kwa kushindwa kuwatokomeza wanamgambo wa kundi la Boko Haram.

XS
SM
MD
LG