Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 19:49

Boko Haram wafanya shambulizi kwenye kijiji cha Dalori


Mtu mmoja anapita kando ya nyumba zilizochomwa kufuatia shambulizi la Boko Haram katika kijiji cha Dalori kilometa 5 kutoka Maiduguri, Nigeria.
Mtu mmoja anapita kando ya nyumba zilizochomwa kufuatia shambulizi la Boko Haram katika kijiji cha Dalori kilometa 5 kutoka Maiduguri, Nigeria.

Walioshuhudia wanasema wanamgambo hao walishambulia kijiji cha Dalori kilichoko karibu na Maiduguri Jumamosi usiku na kuanza kuchoma nyumba na kuwapiga watu risasi

Kundi la wanamgambo la Boko Haram limeshambulia kijiji kilichoko kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuuwa takriban watu 50.

Walioshuhudia wanasema kuwa wanamgambo hao walishambulia kijiji cha Dalori kilichoko karibu na Maiduguri Jumamosi usiku na kuanza kuchoma nyumba na kuwapiga watu risasi.

Mwanajeshi mmoja ameliambia shirika la habari la AP kuwa washambuliaji watatu wanawake wa kujitoa mhanga walijilipua wakiwa miongoni mwa kundi la watu na kusababisha majeraha zaidi. Kundi hilo lilizusha hasira miongoni mwa jumuia ya kimataifa hapo Aprili 2014 pale lilipowateka nyara wasichana 276 kutoka shule moja ya sekondari katika kijiji cha Chibok. Hamsini kati yao waliweza kutoroka lakini zaidi ya 200 hawajulikani walipo hadi leo.

XS
SM
MD
LG