Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 12:18

Boko Haram kudaiwa kuhusika na mauaji Dikwa


Picha hii iliyopigwa Januari 15, 2018, kutoka kwenye video iliyotolewa siku hiyo na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram. Picha na AFP / BOKO HARAM.
Picha hii iliyopigwa Januari 15, 2018, kutoka kwenye video iliyotolewa siku hiyo na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram. Picha na AFP / BOKO HARAM.

Wanamgambo wa Kiislamu wamewauwa takriban watu 25 katika shambulio lililotokea katika mji wa wavuvi wa Dikwa katika jimbo la Borno nchini Nigeria.

Polisi na wakaazi wa eneo hilo walisema Alhamisi. Kamishna wa polisi Abdu Umar amelihusisha shambulio la Dikwa na waasi wa Boko Haram. Ma kuongezea kuwa polisi mmoja aliuawa katika tukio tofauti.

Mji wa Dikwa uko jirani na msitu wa Sambisa, ngome ya Boko Haram, ambao Islamic State ya West Africa Province (ISWAP) inahusika kulipigania eneo hilo.

Bulama Modu, mkaazi wa eneo hilo ambaye analisaidia jeshi katika shughuli za uokozi, amesema jumla ya wavuvi 33 wameuwawa. Amesema miili 25 imepatikana katika eneo la tukio la Juamatano wakati miili mingine nane imepatikana Alhamisi.

Mkaazi mwingine ambaye aliweza kutoroka alisema waasi hao waliwashuku wavuvi kuwa walikuwa wakitoa taarifa kwa jeshi baada ya tukio la wiki kadhaa zilizopita baada ya jeshi kuwasahmbulizi. Waasi walikuwa wakidai fedha kutoka wa wavuvi.

Jeshi halikujibu ombi la kutoa maoni yake. Uasi wa Boko Haram, ambao umezuka kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka 2009, umeua zaidi ya watu 350,000 na kuwalazimisha mamilioni kukimbia makazi yao.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG