Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 06:23

Bodi ya mitihani Malawi yavunjwa baada ya mitihani kuvuja


 Lazarus Chakwera - Rais wa Malawi
Lazarus Chakwera - Rais wa Malawi

Rais wa Malawi ameagiza bodi ya mitihani ya kitaifa nchini humo kuvunjiliwa mbali baada ya mitihani ya kitaifa ya mwaka huu kuvuja na kusambaa kwa mitandao ya kijamii kabla ya watahiniwa kuifanya.

Hatua ya mitihani hiyo kuvuja, ilipelekea mitihani ya kitaifa kuahirishwa na kupelekea wanafunzi kuingia mitaani kwa maandamano, wakikabiliwa na polisi waliowatawanya kwa kutumia gesi ya kutoa machozi.

Akihutubia taifa, rais Lazarus Chakwera amesema kwamba wasimamizi wa bodi ya mitihani nchini humo wanastahili kufutwa kazi kwa kuzembea kazini na kupelekea mitihani ya kitaifa kuvuja.

Agizo lako linajiri siku moja baada ya wizara ya elimu kufutilia mbali mtihani wa kitaifa kwa watahiniwa wa shule za upili, uliokuwa umepangiwa kuanza Oktoba 27.

Rais Chakwera amesema kwamba hatua ya mitihani hiyo kuvuja ni dhihirisho kwamba bodi inayosimamia mitihani ya kitaifa haina uwezo wa kusimamia mitihani nchini humo.

Polisi wamekamata wanafunzi 38 na walimu watatu kutoka shule baada ya kupatikana na karatasi sita za mitihani zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mkurugenzi wa bodi ya mitihani nchini Malawi Gerald Chiunda, ameambia waandishi wa habari kwamba huenda karatasi za mitihani zilivuja kutoka ofisini mwake na kwamba uchunguzi unaendelea.

Rais Chakwera ameamuru waziri wa elimu kuwaadhibu wahusika wote kabla ya mwezi huu wa Novemba kukamilika.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG