Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 20:20

Blinken: nchi zenye nguvu zingeiga mfano kutoka kwa Russia na kushambulia zingine


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken, akiwa katika ziara Afrika kusini Aug 7 2022. Picha: Reuters

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema kwamba endapo hatua hazingechukuliwa dhidi ya Russia baada ya kuivamia Ukraine, nchi nyingine duniani zingeanza kufanya namna Russia ilivyofanya, na kukandamiza nchi nyingine kote duniani.

Blinken alikuwa akizungumza na waandishi wa habari nchini Afrika kusini, ambapo alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini Naledi Pandor, katika ziara yake ya nchi tatu za Afrika, ambapo pia atatembelea Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Rwanda.

Amesema kwamba endapo ulimwengu utaruhusu nchi zenye nguvu duniani kuvamia nchi ndogo itakuwa jambo la kawaida kwa nchi nyingine kufanya hivyo sio tu Ulaya bali kote duniani, bila kuwajibishwa.

Blinken amesema kwamba Marekani inatambua kwamba ni muhimu kuiwajibisha Russia kutokana na uvamizi kwake Ukraine kwa sababu uvamizi huo unatishia misingi ya hali kote duniani.

Russia ilivamia Ukraine Februari tarehe 24 katika kile inakitaka kama operesheni maalum ya kijeshi ili kuwalinda watu wanaozungumza kirusi nchini Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini amesema kwamba hakuna mtu yeyote anaunga mkono vita vinavyoendelea Ukraine lakini mifumo ya sheria ya kimataifa inaonekana kutekelezwa kwa upendeleo, akitaka hatua kama hizo kuchukuliwa ili kuangazia yanayoendelea Palestina

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG