Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 09, 2024 Local time: 01:56

Blinken kuelekea China, kujadili Russia na Ukraine


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, anaelekea Beijing kwa mazungumzo na maafisa wakuu wa China kuhusu masuala ya vita vya Russia na Ukraine, biashara na ushirikiano katika kukabiliana na dawa za kulevya.

Lakini utawala wa Rais Joe Biden unakabiliwa na maswali magumu kutoka kwa wakosoaji wa bunge, kwani matarajio ni madogo kwamba mazungumzo kama haya yataleta matokeo makubwa.

Blinken atakuwa mwanadiplomasia mkuu wa kwanza wa Marekani kwenda China tangu 2018.

Safari fupi ya Beijing haitarajiwi kurekebisha kutokukubaliana baina ya nchi hizo mbili juu ya kile maafisa wa Marekani wanasema ni mazoea ya biashara isiyo ya haki ya China na ujasusi wa kiviwanda, pamoja na vitisho vya Beijing dhidi ya Taiwan.

XS
SM
MD
LG