Blinken alisema uhusiano wa Marekani na Ufilipino ni wa hali ya juu na aliihakikishia Ufilipino utayari wake wa kufanya kazi na taifa la Kusini Mashariki mwa Asia katika maeneo ya ulinzi, mabadiliko ya hali ya hewa na kudhibiti janga la Covid-19.
Blinken, afisa wa juu zaidi wa Marekani kutembelea Ufilipino tangu Marcos apate ushindi wa kishindo mwezi Mei, alithibitisha kujitolea kwa Marekani kwa mkataba wake wa ulinzi wa 1951 na Ufilipino.