Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 12:28

Blinken akutana na Waziri Mkuu wa Qatar


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (Kushoto) akutana na Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani katika kasri ya Lusail nchini Qatar Juni 12 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (Kushoto) akutana na Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani katika kasri ya Lusail nchini Qatar Juni 12 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anakutana Jumatano na Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, huku maafisa wa Marekani, Qatar na Misri wakitathimini jibu la Hamas, kwa pendekezo la kusitisha mapigano Gaza.

John Kirby, mshauri wa masuala ya usalama wa White House, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Hamas iliwasilisha majibu yake kwa Qatar na Misri Jumanne, na kwamba Marekani inadhani jibu hilo lina baraka za kiongozi mkuu wa Hamas huko Gaza, Yahya Sinwar.Kirby alikataa kutoa maelezo mengi, akisema kufanya hivyo kungevuruga mchakato wa mazungumzo.

Kulingana na Hamas na kundi dogo la wanamgambo wa Islamic Jihad, wako tayari "kushughulika ili kufikia makubaliano," wakiweka kipaumbele "kusimamishwa kabisa" kwa vita.

"Majibu ya Hamas yalisisitiza msimamo wa kundi hilo kwamba makubaliano yoyote lazima yasitishe uchokozi wa Wazayuni dhidi ya watu wetu, yatoe majeshi ya Israel, yajenge upya Gaza na kufikia makubaliano mapana ya kubadilishana wafungwa," afisa wa Hamas alisema.

Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza maelezo ya pendekezo la kusitisha mapigano, wakati yeye na maafisa wengine wa Marekani wamesisitiza mara kwa mara kuwa ni pendekezo la Israel.

Blinken alisema Jumanne kwamba Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alithibitisha kujitolea kwake kwa makubaliano hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG