Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller alisema katika taarifa yake kwamba Blinken "kwa mara nyingine alisisitiza kwamba Marekani inaunga mkono hatua zinazoonekana kuelekea kuundwa kwa taifa la Palestina pamoja na Taifa la Israeli, na wote wanaishi kwa amani na usalama."
Blinken pia aliitaka Israeli kuhamishia mapato yote ya kodi ya Wapalestina inazokusanya kwa mamlaka ya Palestina kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo.
Mamlaka ya Palestina inatawala sehemu ya Ukingo wa Magharibi, huku kundi la wanamgambo wa Hamas likidhibiti Ukanda wa Gaza ambako Israeli inapigania kulitokomeza kundi hilo. Marekani imetazamia mpango madhubuti wa baada ya vita, ambao utaiweka Gaza chini ya utawala unaoongozwa na Wapalestina bila jukumu lolote kwa Hamas.
Lakini wachambuzi wengine wana mashaka na matarajio hayo.
Blinken amesisitiza uwezekano wa Israel kukubalika na majirani wake wa Kiarabu kwa kutafuta njia kuelekea kuanzisha taifa la Palestina kama njia ya kutatua mzozo huo.
Netanyahu amekataa katakata suluhisho la mataifa mawili.
Forum