Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 27, 2025 Local time: 13:13

Blinken akamilisha ziara Israel


APTOPIX Israel Palestinians US
APTOPIX Israel Palestinians US

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, amemaliza ziara iliyokuwa na hisia ya Israel, ambapo amesema msaada wa Marekani kwa taifa hilo la kiyahudi hautasita, kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa Hamas, ambayo yameuwa mamia ya Waisrael.

“Ujumbe ninaoleta Israel ni huu, kwamba mnaweza kuwa madhubuti kikamilifu wenyewe kujilinda, lakini kwa kuwa Marekani, ipo kamwe hamtakuwa peke yenu, alisema waziri Blinken, akiwa pembeni ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, mjini Tel Aviv.

Waziri Blinken, aliulizia picha ambazo waziri mkuu Netanyahu alimuonyesha za watoto, na vijana waliouwawa katika shambulizi hilo lililotajwa kuwa la kigaidi la Hamas. Waziri Blinken alisema picha hizo zinatisha na kusikitisha.

Forum

XS
SM
MD
LG