Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 15, 2024 Local time: 19:59

Blinken aelekea Mashariki ya Kati kwa mara nyingine


Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani Antony Blinken.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani Antony Blinken.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anaelekea Riyadh kwa mazungumzo ya kikanda Jumatatu na Jumanne kuhusu usaidizi wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, mipango ya baada ya vita, kwa maeneo ya Palestina, na utulivu na usalama katika Mashariki ya Kati.

"Waziri atajadili juhudi zinazoendelea za kufikia makubaliano ya usitishaji vita huko Gaza ambao utafanikisha kuachiliwa kwa mateka na jinsi Hamas inavyosimama kati ya watu wa Palestina na kusitisha mapigano," Wizara ya Mambo ya Nje ilisema.

Blinken atahudhuria mkutano wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba, muungano wa kikanda wa nchi za Kiarabu zinazopakana na Ghuba ya Uajemi unaofanyika katika mji mkuu wa Saudi Arabia.

Msemaji wa usalama wa taifa wa White House John Kirby aliambia kipindi cha "Wiki Hii" cha shirika la habai la ABC Jumapili kwamba Marekani inaendelea kushinikiza kusitishwa kwa mapigano kwa wiki sita katika vita vya takriban miezi saba huko Gaza, kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.

Forum

XS
SM
MD
LG