Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 21:08

Burundi yabadili uamuzi juu ya chanjo ya Covid 19


Rais wa Burundi Evariste Ndayshimiye, wakati wa kampeni alipokuwa akigombea kiti cha uongozi wa wa chama tawala cha CNDD-FDD Gitega, Burundi, Mei 20,2020.
Rais wa Burundi Evariste Ndayshimiye, wakati wa kampeni alipokuwa akigombea kiti cha uongozi wa wa chama tawala cha CNDD-FDD Gitega, Burundi, Mei 20,2020.

Serikali ya Burundi sasa inasema itakubali chanjo za COVID-19, na kuwa moja ya nchi ya mwisho ulimwenguni kupokea hiyo chanjo

Serikali ya Burundi sasa inasema itakubali chanjo za COVID-19, na kuwa moja ya nchi ya mwisho ulimwenguni kupokea. Lakini wizara ya afya nchini humo inasema haitachukua jukumu la athari yoyote ambayo inaweza kusababishwa na chanjo.

Waziri wa Afya Thaddee Ndikumana Jumatano alisema chanjo hizo zitafika kwa msaada wa Benki ya Dunia. Haikufahamika mara moja nchi hiyo itapokea dozi ngapi au lini.

Chanjo hiyo itapewa wale wanaohitaji, waziri wa afya alisema. Serikali itahifadhi chanjo lakini haitawajibika kwa athari yoyote ameongeza.

Tangazo la Burundi lilikuja siku hiyo hiyo ambayo nchi jirani ya Tanzania ilizindua kampeni yake ya chanjo, ikibadili mwelekeo kutoka kwa Rais wa zamani John Magufuli kukataa kutambua kuwepo kwa janga hilo. Alifariki mwezi Machi na urais ulikwenda kwa makamu wake Samia Suluhu Hassan, ambaye tangu wakati huo amebadili mwelekeo wa kupambana na COVID-19 katika moja ya nchi zenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Rais wa Burundi hayati Pierre Nkurunziza, ambaye alifariki mwaka jana, pia alikosolewa kwa kudharau janga hilo. Utawala wa mrithi wake, Rais Evariste Ndayishimiye, mapema mwaka huu ulisema nchi hiyo ya watu zaidi ya milioni 11 bado haihitaji chanjo za COVID-19.

XS
SM
MD
LG