Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 16, 2025 Local time: 12:22

Bishara katika soko la fedha la Wall Street ilishuka Jumatatu


Mfano wa masoko ya fedha katika Wall Street
Mfano wa masoko ya fedha katika Wall Street

Mshtuko wa masoko ya fedha umetokea China ambapo kampuni moja imetengeneza app inayoshindana na kampuni kubwa za Marekani

Biashara ya Wall Street ilishuka Jumatatu kwa hofu kuwa makampuni makubwa ya Marekani ambayo yameshiriki katika biashara ya akili mnemba (AI) yanakabiliwa na kitisho kutoka kwa mshindani nchi ya China ambayo inaweza kufanya mambo kama hayo kwa bei nafuu zaidi. S&P 500 ilikuwa chini ya asilimia 1.9 mwanzoni mwa biashara.

Hisa za Tech ambazo zimekuwa nyota kubwa za soko zilichukua hasara kubwa zaidi, wakati Nvidia ilishuka chini ya asilimia 11.5, ikifuatiwa na Nasdaq ilishuka kwa asilimia 3.2. Kwa upande wa Dow Jones ambayo iko chini kwenye teknolojia, ilipanda juu kidogo kwa pointi 160, au asilimia 0.4 kuanzia asubuhi ya leo Jumatatu.

Mshtuko wa masoko ya fedha umetokea China ambapo kampuni inayoitwa DeepSeek ilisema imetengeneza program kubwa ya lugha ambayo inaweza kushindana na kampuni kubwa za Marekani lakini kwa gharama ndogo.

Programu ya DeepSeek tayari imepata umaarufu kwenye duka lenye Programu za Apple mapema Jumatatu, na wachambuzi walisema kuwa kazi kama hiyo itakuwa ya kuvutia kutokana na namna serikali ya Marekani imeizuia China kuwa na fursa ya kuingiza program zake za AI.

Forum

XS
SM
MD
LG