Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 03:27

Bingwa wa dunia wa Marathon Kelvin Kiptum afariki katika ajali ya barabarani


Picha ya Maktaba: Kelvin Kiptum baada ya kushinda Chicago Marathon mwaka 2023.
Picha ya Maktaba: Kelvin Kiptum baada ya kushinda Chicago Marathon mwaka 2023.

Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za marathon Kelvin Kiptum na kocha wake Gervais Hakizimana walifariki katika ajali ya barabarani siku ya Jumapili, Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Waziri wa michezo wa Kenya, Ababu Namwamba alisema kwenye X , "Inauma sana!! Kenya imepoteza mtu mwenye thamani maalum. Sijui nisema nini."

Kiptum, aliyekuwa na umri wa miaka 24, aliweka rekodi ya dunia katika mbio za Chicago Marathon, mwezi Oktoba mwaka jana, kwa muda wa saa mbili na nukta 35 na kuvunja rekodi ya iliyokuwa imewekwa na mwenzake Eliud Kipchoge mjini Berlin mnamo mwaka 2022.

Kiptum alivunja rekodi ya London Marathon mapema mwaka jana na alidhamiria kufanya vivyo hivyo tena mjini Chicago, ambako alikimbaia umbali wa kilomita 35 kabla ya kuinua mikono yake hewani huku akishangiliwa na umati wa watu chini hadi pale aliposhinda mbio hizo.

Forum

XS
SM
MD
LG