Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:31

Bin Laden alitaka rais Obama auwawe


Rais Obama na maafisa wa juu wa Marekani katika White House Mei 1, 2011
Rais Obama na maafisa wa juu wa Marekani katika White House Mei 1, 2011

Gazeti la Washington Post limeripoti njama za Bin Laden dhidi ya rais Obama

Gazeti la Marekani Washington Post linaripoti kuwa gaidi Osama Bin Laden alikuwa ameagiza mtandao wake wa al-Qaida kumuuwa rais wa Marekani Barack Obama na jenerali David Petraeus ambaye wakati huo alikuwa kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Marekani nchini Afghanistan.

Mwandishi wa wa gazeti hilo David Ignatius aliripoti Ijumaa kuwa hati zilizopatikana katika uwanja wa Bin Laden zilielezea jinsi hatua hizo zingechukuliwa.Bin Laden aliandika kuwa kumwua rais Obama kutahakikisha makamu rais Joe Biden ataingia madarakani, mtu ambaye Bin Laden alielezea kuwa atakuwa hajajiandaa kuingia katika wadhifa huo.

Bin Laden alimtaka gaidi wa Pakistan Ilyas Kashmiri afanye shambulizi hilo dhidi ya rais wa Marekani. Kashmiri aliuawa na ndege ya Marekani isiyoongozwa na rubani mwezi Juni mwaka wa jana.

Lakini maafisa wa Marekani na wachambuzi wanasema hakuna ushahidi al-Qaida ilikuwa imekaribia kufanya mashambulizi yaliyopendekezwa na kiongozi wao. Osama Bin laden aliuawa na makamanda wa kikosi maalum cha Marekani tarehe 2 Mei mwaka jana katika mji wa Abbottabad nchini Pakistan.

XS
SM
MD
LG