Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:02

Bill Clinton amsifu mkewe katika hotuba ya DNC


Rais Bill Clinton akizungumza katika siku ya pili ya mkutano wa DNC mjini Philadelphia, Pennsylvania July 26, 2016
Rais Bill Clinton akizungumza katika siku ya pili ya mkutano wa DNC mjini Philadelphia, Pennsylvania July 26, 2016

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton mume wa mgombea kiti cha rais wa chama cha Demokratik, Hillary Clinton, usiku wa Jumanne alishangiliwa alipohutubia mkutano mkuu wa chama hicho unaoendelea mjini Philadelphia, jimbo la Pennsylvania.

Katika hotuba iliyojawa na hamasa, Bwana Clinton aliwarai wapiga kura kumchagua mkewe wakati wa uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu.

Alianza hotuba yake kwa kueleza jinsi walivyokutana kwa mara ya kwanza kabisa na kusifu uhusiano wao wa hadi hii leo. Hotuba ya Bwana Clinton ilikuwa kilele cha siku ya pili ya mkutano huo ambao pia ulihutubiwa na viongozi kadhaa na wafuasi wengine wa Bi Clinton.

Rais Clinton awafurahisha wajumbe wa chama kwa hotuba ya kusisimua
Rais Clinton awafurahisha wajumbe wa chama kwa hotuba ya kusisimua

Huku akishangiliwa na umati uliosimama kwa heshima yake, rais huyo wa 42 wa Marekani alimtaja Hillary Hillary kama “rafiki yangu mkubwa ambaye hafi moyo kwa changamoto zozote.”

Alitoa sababu nyingi ambazo alisema ndizo zinamfanya Bi Clinton kuwa tayari kuwa rais.

"Ninamjua kama mtu ambaye hutafuta suluhisho kwa tatizo lolote, popote alipo," alisema.

Saa chache awali, Hillary Clinton alikuwa ametangazwa rasmi kama mwanamke wa kwanza nchini Marekani kuidhinishwa kuwania urais na chama kikubwa Marekani.

Kupitia video iliyorekodiwa, Bi Clinton alikuwa wa mwisho kabisa kuzungumza katika siku ya pili ya kongamano hilo na kuwashukuriu wajumbe kwa kumetua kua mgombea wao.

“Iwapo kuna wasichana wadogo huko ambao hawajalala na wananitazama, ningependa kuwaambia, huenda nikawa rais wa kwanza mwanamke Marekani na mmoja wenu anaweza kunifuata,” alisema.

Awali, katika kile kilichokusudiwa kuashiria umoja ndani ya chama cha Demokratik, aliyekuwa mpinzani wa Clinton, Seneta Bernie Sanders, aliuambia mkutano huo kuwa alitaka kanuni zake zisitishwe kwa muda ili waliohudhuria wamuidhinishe kwa sauti ya pamoja, tofauti na ilivyokuwa miaka nane iliyopita wakati bi Clinton alikaribia kipaza sautina kumuidhinisha mpinzani wake wakati huo, rais wa sasa, Barack Obama. Uteuzi huo umefanyika baada ya wajumbe wa majimbo yote 50 kushiriki katika upigaji kura kwa sauti Jumanne jioni, na kura 15 za ujumbe wa Dakota Kusini zilimhakikishia kupata zaidi ya kura 2, 383 zinazohitajika ili kuweza kuteuliwa rasmi.

Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nchi za nje atatoa hotuba yake siku ya Alhamisi ambapo anatarajiwa kukubali rasmi uteuzi huo.

XS
SM
MD
LG