Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 09, 2024 Local time: 04:43

Bilionea Smith atawalipia deni la shule wahitimu wa Morehouse 2019


Wahitimu chuo cha Morehouse huko Atlanta, Georgia, Mei 19, 2019.
Wahitimu chuo cha Morehouse huko Atlanta, Georgia, Mei 19, 2019.

Robert Smith ni m-Marekani mweusi wa kwanza kutia saini mkataba ujulikanao The Giving Pledge kampeni iliyoanzishwa na Bill ma Melinda Gates pamoja na Warren Buffet ambayo inawahamasisha matajiri duniani kutoa sehemu kubwa ya utajiri wao kwa ajili ya kazi za ufadhili wa mambo mbali mbali

Takribani wahitimu 400 wa chuo cha Morehouse cha wavulana pekee kilichopo mji wa Atlanta kwenye jimbo la Georgia nchini Marekani walipata zawadi ya kushtukiza kutoka kwa bilionea mwekezaji wa teknolojia Robert Smith kwamba atawalipia wanafunzi hao wa darasa la mwaka 2019 madeni ya shule yaliobaki.

Smith ambaye alikuwa mzungumzaji mkuu kwenye sherehe za chuo hicho binafsi cha watu weusi Marekani ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Vista Equity Partners kampuni binafsi inayowekeza katika vifaa vya kompyuta, takwimu na makampuni yanayohusika na teknolojia.

Bilionea Robert Smith akizungumza kwenye mahafali ya chuo cha Morehouse
Bilionea Robert Smith akizungumza kwenye mahafali ya chuo cha Morehouse

Bilionea huyo alishatangaza zawadi ya dola milioni 1.5 kwa shule hiyo ya Morehouse kabla ya sherehe za wahitimu kuanza. Ahadi ya Jumapili kuwafutia madeni wanafunzi wa darasa la mwaka 2019 inakadiriwa kugharimu kiasi cha dola milioni 40. Katika kuongezea utoaji wa zawadi hiyo Smith alisema anatarajia washiriki hao watasonga mbele na mipango mizuri ya maisha yao ya baadae.

Rais wa chuo cha Morehouse, David A. Thomas alisema kuwa wanafunzi wengi wana nia ya kusomea ualimu lakini jambo la kumaliza shule huku wakiwa na mzigo mkubwa wa deni unafanya ndoto zao kutotimia. Hii ilikuwa ni zawadi ya kutoa hamasa kwa vijana hao wa kiume ambayo imefungua njia kwenye maisha yao.

XS
SM
MD
LG