Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:55

"Bila ya majadiliano uvamizi hautaweza kusitishwa" - Zelensky


Wanajeshi wa Rashia katika mji wa kusini wa Mariupol, Ukraine
Wanajeshi wa Rashia katika mji wa kusini wa Mariupol, Ukraine

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine, amerudia tena kusema kwamba yuko tayari kuwa na mazungumzo na mwenzake Vladimir Putin wa Rashia, akisisitiza kwamba bila ya majadiliano hawataweza kusitisha mapigano.

Mapigano makali yakiendelea katika pembe mbali mbali za Ukriane, Rais Volodymyr Zelensky amerudia tena kusema kwamba yuko tayari kuwa na mazungumzo na mwenzake Vladimir Putin wa Rashia, akisisitiza kwamba bila ya majadiliano hawataweza kusitisha mapigano.

Katika hotuba yake siku ya Jumapili, Zelensky amesema mazungumzo yanayoendelea kati ya Kyiv na Moscow tangu Rashia kuivamia Ukraine Februari 24 hayajaleta maendeleo bado lakini anasema ni muhimu kuendelea kuzungumza.

Alipokua anatoa hotuba yake, maelfu ya wakazi wa nchi yake wamekua wakikimbia kupitia vituo vinane vilivyopangwa kuwa njia ya usalama kuelekea nchi jirani.

Nae kamishna mkuu wa Shirika la la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi Filippo Grandi, amesema pia Jumapili, kwamba karibu watu milioni 10, ikiwa ni robo ya wakazi wa Ukraine wamekimbia kutoka nyumba zao kutokana na uvamizi wa Rashia unaosababisha uharibifu mkubwa.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Grandi amesema, kati ya watu hao wote million 10, milioni 3.3 wamekimbilia nchi jirani na karibu milioni 6 wamebaki ndani ya nchi.

UNHCR inasema kwamba asili mia 90 ya waukraine walokimbia ni wanawake na watoto, huku wanaume kati ya miaka 18 hadi 60 wamelazimishwa kubaki kulinda nchi yao.

Kwa upande wa kidiplomasia, Uturuki imesema hii leo kwamba Rashia na Ukraine zimefanya maendeleo kwenye mazungumzo yao kusitisha uvamizi na pande hizo mbili ziko karibu ya kufikia makubaliano.

Ankara inasema iko tayari pia kuanda mkutano kati ya Rais Zelensky wa Ukraine na mwenzake Putin wa Rashia. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.

Wakati huo huo, maandamano ya kuwaunga mkono Waukraine yamefanyika katika miji mbali mbali ya nchi za Ulaya na Marekani hii leo, kudai kusitishwa mara moja, uvamizi wa Rashia huko Ukraine.

XS
SM
MD
LG