Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 22:42

Biden na Netanyahu wajadiliana kuhusu Gaza


(Picha ya Maktaba) Rais wa Marekani Joe Biden akiwa katika mkutano na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
(Picha ya Maktaba) Rais wa Marekani Joe Biden akiwa katika mkutano na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Rais wa Marekani, Joe Biden, na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walijadili kuhusu maendeleo ya vita Gaza.

Malori 14 ya ziada yalivuka kituo cha mpaka cha Rafah yakibeba na kuwasilisha misaada mbalimbali ya kibinadamu mpaka Gaza.

Vita vya Israel, na Hamas, katika siku yake ya 16, vimekuwa ni vibaya zaidi kati ya vita vitano vya Gaza, vilivyowahi kutokea siku za nyuma.

Zaidi ya watu 1,400 nchini Israel wameuawa, haswa katika shambulio la awali la Hamas, la Oktoba 7.

Wizara ya afya ya Palestina, imesema idadi ya waliofariki dunia Gaza, imefikia watu takribani 4,651, huku wengine 14,254 wakijeruhiwa. Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alitembelea wanajeshi walioko karibu na mpaka na Lebanon.

Forum

XS
SM
MD
LG