Gari hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi saa za asubuhi siku ya siku kuu ya mwaka mpya. Biden alianza kwa ziara ya kushtukiza kwenye hema la muda la makumbusho karibu na eneo la tukio. Jill Biden aliweka shada la maua kwenye eneo hilo wakati Biden akionyesha ishara ya mslaba.
Baada ya hapo walielekea kanisani ili kukutana na familia za waathirika. “Nafikiri mtakachokiona leo ni rais wenu akishirikiana na jamii wakati huu mgumu,’ msejami wa White House Karine Jean-Pierre, alisema Jumatatu akiwa kwenye ndege ya Airforce One, wakielekea Louisiana.
Shamsud –Din Jabbar ambaye alikuwa mwanajeshi wa Marekani mwenye umri wa miaka 42 kutoka Houston, Texas aliendesha gari hilo kwenye barabara ya Bourbon mjini New Orleans, eneo lenye watalii wengi na kusababisha maafa hayo.
Biden ambaye amebakisha wiki 2 ofisini pia anakutana na wachunguzi ambao wamesema kwamba Jabbar alifanya shambulizi hilo akiwa pekee yake, lakini anaaminika kuwa na ushawishi wa kundi la Islamic State. Idara ya FBI imesema kuwa Jabbar aliweka video 5 kwenye mitandao ya kijamii takriban saa moja kabla ya kufanya shambulizi hilo, akieleza uungaji mkono wake kwa Islamic State.
Forum