Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:34

Biden kutembelea waathirika wa mauaji , New York


Rais wa Marekani Joe Biden na mke wake Jill Biden kwenye picha ya awali.
Rais wa Marekani Joe Biden na mke wake Jill Biden kwenye picha ya awali.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne anatarajiwa kuwataka wamarekani kukemea chuki ya aina yoyote pamoja na kulishi bunge kupitisha sheria za kudhibiti umiliki wa bunduki.

Hao yanajiri wakati yeye na mke wake Jill Biden wakielekea New York ili kutoa pole zao kwa watu walioathiriwa na mauaji ya bunduki yaliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye kitongoji cha Buffalo. Biden na mkewe wanatarajiwa kutembelea eneo la kumbukumbu na pia kukutana na familia za waathirika, maafisa wa usalama, waokozi pamoja na viongozi wa kieneo.

Payton Gendron ambaye ni mwanaume wa kizungu mwenye umri wa miaka 18 aliwaua watu 10 kwa kuwapiga risasi huku wengine watatu wakiachwa na majeraha walipokuwa kwenye duka moja la vyakula kwenye kitongoji cha Buffalo chenye wakazi wengi weusi.

Kumi na mmoja kati ya waliopigwa risasi walikuwa ni watu weusi. Idara ya upelelezi ya FBI inaendelea kuchunguza tukio hilo wakati pia ikipitia makala yenye kurasa 180 iliyoandikwa na Gendron ikisemekana kuwa na maneno yenye chuki dhidi ya watu wasio wazungu, pamoja na wasio wa kristo. Gendron sasa hivi amezuiliwa na polisi baada ya kujisalilisha muda mfupi baada ya kutekeleza mauaji hayo.

XS
SM
MD
LG