Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 21:26

Biden kutembelea mashariki ya kati inayopitia mabadiliko makubwa ya siasa


Rais wa Marekani Joe Biden akishuka Air Force One baada ya kuasili katika uwanja wa ndege wa Franz-Josef-Strauss karibu na Munich, Ujerumani, June 25, 2022. PICHA: AP
Rais wa Marekani Joe Biden akishuka Air Force One baada ya kuasili katika uwanja wa ndege wa Franz-Josef-Strauss karibu na Munich, Ujerumani, June 25, 2022. PICHA: AP

Rais wa Marekani, Joe Biden anatarajiwa kwenda Mashariki ya Kati wiki ijayo, eneo ambalo linapitia mabadiliko makubwa ya siasa za kieneo.

Itakuwa ni ziara ya kwanza ya Joe Biden huko Mashariki ya Kati kama Rais wa Marekani ambayo inakujakatika kipindi muhimu sana kwa wote Saudi Arabia na Iran katika uwanja wa kimataifa.

Mwana mfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman amerejea hivi karibuni kutoka ziara yake nchini Misri, Uturuki na Jordan wakati ufalme huo ukijaribu kufanya marekebisho ya uhusiano wake wa kimataifa.

Profesa Simon Mabon katika siasa za kimataifa kwenye Chuo Kikuu cha Lancaster anasema “Saudi Arabia imesukumwa pembeni kwenye jumuiya ya kimataifa, kwa upande mmoja kutokana na mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, lakini kwa upande mwingine ni vita vinavyoendelea nchini Yemen, ambavyo vimekuwa na athari kubwa sana kwa binadamu. Kwahiyo inachofanya Saudi Arabia hivi sasa ni kujiingiza katika uwanja wa kimataifa.”

Umuhimu wa ziara ya Biden

Ziara ya Biden huko Riyadh inaashiria uwazi kutoka Washington.

Profesa Mabon anasema mengi yanahusu kile ambacho kinaendelea nchini Ukraine, na mafuta na gesi na kupanda kwa bei za bidhaa. Saudi Arabia ameongezea ni mzalishaji mkuu na anaweza kuwa na ushawishi mkubwa sana katika masoko ya dunia.

Iran pia inajaribu kuingia tena katika uwanja wa kimataifa wakati ikifanya mashauriano ya kurejea kwenye makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015, kwa mabadilishano kuwa Marekani itaondoa vikwazo.

“Serikali ya Iran inahitaji sana fedha, “ anasema Profesa Mabon.

Mazungumzo ya Nyukilia

Maendeleo katika mazungumzo ya nyukilia yamekwama, ingawaje, kunamaonyo ambayo yametolewa kwamba program ya Iran yakusindika uraniuam inasonga mbele kwa haraka Zaidi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Ned Price amesema “program ya iran imesonga mbele kwa njia ambazo kwa jumla inatutia wasi wasi mkubwa.”

Iran Saudi Arabia wamekuwa katika mapambano katika vita huko nchini Yemen tangu mwaka 2014, nchi hizo mbili zilivunja mahusiano mwaka 2016. Sitisho la mapigano la mwezi Machi kati ya wahouthi wanaoungwa mkono na Iran na serikali ya Yemen ambayo inaungwa mkono na Saudi Arabia bado linaendlea.

Tehran na Riyadh wamefanya duru ya tano ya mazungumzo mjini Baghdad mwezi April kwa lengo la kupunguza mivutano na kufanya mazungumzo zaidi ambayo yamepangwa.

Biden kutembelea Israel na maeneo ya wapalestina

Kabla ya Riyadha, Biden kwanza atakwenda Israel na maeneo ya wapalestina ambako matarajio ya ziara ya huko yako chini.

Wakati huo huo makundi ya kuteteahaki yamemsihi Biden kuzungumzia suala ya haki za binadamu wakati wa ziara yake nchini Saudi Arabia na Israel. Washington ilisema kuwa haki za binadamu ni kiini cha sera ya mambo ya nje ya Marekani.

XS
SM
MD
LG