Upatikanaji viungo

Jumatatu, Agosti 15, 2022 Local time: 18:31

Biden kualika viongozki wa Afrika Washington DC


Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Jumatano ametangaza kwamba Marekani itawaalika viongozi kutoka barani Afrika kwenye kongamano litakalofanyika mwezi  Decemba.

Kongamano hilo litafanyikia Washington ili kujadili changamoto zilizopo kama vile usalama wa chakula na mabadiliko ya hali ya hewa. Katika taarifa yake Biden amesema kwamba, " Kongamano hilo litaonyesha nia ya dhati ya Marekani kwa bara la Afrika katika kuimarisha umuhimu wa uhusiano kati ya Marekani na Afrika na kuongeza ushirikiano katika vipaumbele vya ulimwengu."

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, tangazo hilo limetolewa sambamba na lile la makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris kwa njia ya mtandao wakati wa kongamano la kibiashara kati ya Marekani na Afrika, linaliofadhiliwa na baraza la biashara la Afrika, pamoja na ufalme wa Morocco.

Afisa wa ngazi ya juu kwenye serikali ya Marekani, na ambaye hakutaka kutajwa amesema kwamba takriban viongozi 50 wa Afrika, wanatarajiwa kwenye kongamano hilo litakalo fanyika kati ya Decemba 13-15 hapa mjini Washington DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG