Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 13:04

Obama amtunukia Biden medali ya juu kuliko zote


Rais Barack Obama akimvisha medali Makamu Rais Joe Biden. Jan. 12, 2017.
Rais Barack Obama akimvisha medali Makamu Rais Joe Biden. Jan. 12, 2017.

Rais wa Marekani Barack Obama Alhamisi alimshitukiza Makamu Rais Joe Biden kwa kumtunukia nishani ya juu kuliko zote za urais inayotolewa kwa wananchi: Medali ya Rais ya Uhuru.

Katika kile kilichoitwa kuwa ni “tafrija ya kuagana,” Obama alitangaza medali hiyo kwa makamu wa rais mbele yake katika tafrija hiyo.

“Ikiwa namalizia muda wa mwisho wa urais, ninafuraha kukutunukia medali ya taifa yenye hadhi ya juu kwa mwananchi kuliko zote – Nishani ya Rais ya Uhuru.

Obama alimsifia Biden, seneta wa muda mrefu wa Marekani aliyetokea Delaware, kwa miaka mingi ya uchapaji kazi kwa taifa. Alimpongeza Biden kwa maneno yake rais, “ imani kwa wamarekani wenzako, kwa upendo wako kwa taifa na utendaji wako kwa kipindi cha maisha yako yote ambao athari zake zitaendelea kwa vizazi vijavyo.”

Akijibu hotuba hiyo, Biden ambaye alitokwa na machozi aliishukuru familia yake kwa msaada wao wote na kumpongeza rais kwa kazi yake. Biden alimwagia sifa Obama kwa "uadilifu, maadili na kwa maneno ya Biden, kuwa na hisia na shida za binadamu wenzie,” akisema hajawahi kumjua rais mwengine ambaye alikuwa na sifa hizi.

Katika maoni yake, Biden pia amesema kuwa anapotajwa kwa kuhusishwa na uongozi wa Obama, atakuwa na fahari kubwa “ kwamba naweza kusema nilikuwa sehemu ya safari hii ya mtu bora aliyefanya mambo bora kwa nchi yake".

XS
SM
MD
LG