Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 02:18

Biden atumia hotuba yake kueleza maadili ya taifa ndani na nje ya Marekani


Rais wa Marekani Joe Biden akilihutubia taifa. Nyuma yake ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi na Makamu wa Rais Kamala Harris. Picha ya AFP
Rais wa Marekani Joe Biden akilihutubia taifa. Nyuma yake ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi na Makamu wa Rais Kamala Harris. Picha ya AFP

Rais Joe Biden katika hotuba yake ya kwanza juu ya hali ya kitaifa Jumanne usiku alikuwa na maneno mazito kwa wapinzani wake wa kimabavu na kutoa faraja kwa watu ambao wanapambana, waliopigwa na janga baya la COVID-19, ongezeko la bei na migawanyiko mibaya ya kisiasa.

Katika hotuba yake, Biden alisisitiza wakati wote maadili yale yale aliyowasihi Wamarekani kukumbatia kama alivyosema katika hotuba yake wakati wa kuapishwa: Umoja.

“Sisi ni taifa pekee duniani ambalo siku zote tumeweza kubadilisha migogoro tuliyokabiliwa nayo kuwa ni fursa,” Biden alisema katika kuhitimisha hotuba yake ya takriban saa moja ambayo iligusia masuala mbalimbali kuanzia mgogoro wa Ukraine mpaka uchumi wa Marekani, janga la corona, na mageuzi ya sheria katika maeneo kama haki za umiliki wa bunduki na haki za kupiga kura.

“Hivi leo tuko imara zaidi kuliko tulivyokuwa mwaka mmoja uliopita. Na tutakuwa imara zaidi mwaka mmoja kutoka sasa kuliko tulivyo leo. Huu ni wakati wa kukutana na kuzishinda changamoto za wakati wetu.”

Angazio la Ukraine

Wakati wabunge wa Bunge la Marekani wakipeperusha bendera za rangi ya bluu na manjano za Ukraine, Biden hakupoteza muda kuzungumzia vita vinayvoongezeka kati ya Russia na Ukraine, akitangaza kuwa alikuwa anafunga mara moja anga za Marekani kwa ndege za Russia. Aliendelea kuzungumzia suala hilo kwa dakika nyingine 10.

Rais Joe Biden akitoa hotuba yake ya kwanza ya hali ya kitaifa katika kikao cha pamoja cha Bunge la Marekani - Congress huko Capitol, Machi 1, 2022, Washington.(Shawn Thew/Pool via AP).
Rais Joe Biden akitoa hotuba yake ya kwanza ya hali ya kitaifa katika kikao cha pamoja cha Bunge la Marekani - Congress huko Capitol, Machi 1, 2022, Washington.(Shawn Thew/Pool via AP).

“Siku sita zilizopita, Vladimir Putin wa Russia alitaka kutikisa misingi ya ulimwengu huru akifikiria anaweza kupindisha kwa njia zake ovu, “ alisema, kwa kile kilichoonekana kupongezwa na wote waliokuwepo katika mkusanyiko huo wa Wademokrat na Warepublikan. “Lakini alifanya mahesabu mabaya. Alidhani anaweza kuingia Ukraine na dunia itakubaliana naye. Badala yake alikutana na ukuta wa ujasiri ambao hajawahi kuufikiria. Alikutana na wananchi wa Ukraine.”

Akisisitiza hilo, Oksana Markarova, balozi wa Ukraine nchini Marekani, aliungana na Jill Biden, mke wa Rais katika sehemu aliyokaa kushuhudia hotuba hiyo, na alikaribishwa kwa makofi ya pongezi. White House imesema kuwa mke wa rais alikuwa na nakshi ya ua la alizeti, ikiwa ni ua la taifa, lilikuwa katika kiganja cha nguo yake ya rangi ya bluu iliyokoza iliyotayarishwa kwa ajili ya hotuba hiyo.

Katika hotuba yake Rais Biden alinadi mafanikio yake kwa kuziunganisha nchi nyingi dhidi ya uvamizi wa Rais wa Russia Vladimir Putin huko Ukraine. Biden amesema Ukraine iko mstari wa mbele katika vita yva dunia kati ya demokrasia na udikteta, na kuwa demokrasia itashinda.

Rais Vladimir Putin (Photo by Alexey NIKOLSKY / SPUTNIK / AFP)
Rais Vladimir Putin (Photo by Alexey NIKOLSKY / SPUTNIK / AFP)

Wakati Putin akishambulia miji mikubwa ya Ukraine kama vile Kharkiv na Kyiv, Biden alisimama katika ukumbi wa Bunge na kuwaambia Wamarekani nchi huru duniani zimeungana dhidi ya uchokozi wa Putin.

“Ulimwengu huru unamwajibisha, “Biden alisema. “Ikiwa ni pamoja na nchi wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya, ikiwemo Ufaransa, Ujerumani, Italia, na pia nchi kama Uingereza, Canada, Japan, Korea, Australia, New Zealand, na wengine wengi, hata Uswizi imewaletea maumivu Russia na kuwaunga mkono watu wa Ukraine. Putin hivi sasa ametengwa na ulimwengu kuliko alivyowahi kutengwa huko nyuma.”

XS
SM
MD
LG