Modi amekua akikosolewa kwa ukiukaji wa haki za watu wa india walio wachache, huku mashirika ya kutetea haki za binadam yakidai kwamba Rais huyo wa India amefumbia macho ghasia zinazofanywa na wanamgambo dhidi ya waislamu na wakristo nchini humo. Rais wa Marekani Biden amempokea kwa heshima za kitaifa waziri huyo mkuu White House ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na India na kuuzuia ushawishi wa China duniani.
Viongozi hao wanatarajiwa kusaini makubaliano kadhaa kwenye sekta ya ulinzi na biashara.
Biden alimkaribisha ModiWhitehouse mbele ya watu 7,000, na baadaye watakuwa na mazungumzo katika ofisi ya rais na kujumuika pamoja kwa chakula cha jioni.
“Changamoto na fursa zinaoikabili dunia zinahitaji ushirikiano wa India na Marekani na kuongoza pamoja, na tunafanya hivyo," alisema Biden.
Modi amesema ziara hiyo ni heshima kubwa kwa India na wanainchi wake na wanadiaspora wote wa India.
“Hafla hii kubwa ya kunikaribisha White House ni heshima kwa raia bilioni 1.4 wa India, Modi amesema, akiongea Kingereza na Kihindi.
Ameongeza pia kuwa mapokezi hayo pia ni heshima kwa zaidi ya watu milioni 4 wenye asili ya India waishio Marekani.
Forum