Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:04

Biden arai wamarekani kupokea chanjo


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu ametoa wito mpya kwa watu wa Marekani  kupokea chanjo dhidi ya  virusi vya corona au hata kupata chanjo ya tatu maarufu booster, iwapo tayari wamepokea chanjo kamili. 

Tangazo hilo linafuatia ushauri wa mshauri wa juu wa afya wa Marekani, kwamba aina mpya ya virusi vya corona vinavyojulikana kama omicron, kwa hakika huenda vikaingia nchini.

Baiden wakati akitoa hotuba fupi iliyoonekana kulenga takriban watu milioni 60 ambao hawajapokea chanjo Marekani alisema, “Hakuna haja ya kusubiri, kama hujapata chanjo nendeni mpate chanjo sasa hivi.” Hata hivyo Biden amesema kwamba kwa sasa anaamini hakuna haja ya kufunga biashara na shule kutokana na tishio la omnicron.

Ameongeza kusema kwamba utawala wake utafanya kila uwezalo kukabiliana na kirusi hicho kipya, lakini wataalam wa afya walielezea matumaini yao kwamba watu waliochajwa wana kinga ya aina fulani, huku utafiti wa kina wa kisayansi ukiendelea kufanywa. Virusi hivyo ambavyo awali vilitangazwa na Afrika Kusini, hivi sasa vimegunduliwa kwenye mataifa kadhaa ya Ulaya, Asia na Australia.

XS
SM
MD
LG