Kikao hicho pembeni ya mkutano wa viongozi wa nchi saba zenye uchumi mkubwa duniani, mjini Hiroshima, Japan, viongozi hao wamezungumzia tishio la silaha za nyuklia la Korea kaskazini na ushawishi wa China unaoongezeka.
Taarifa ya White House imesema kwamba viongozi hao wamejadiliana namna ya kuimarisha uhusiano wao wa kiusalama kutokana na tichio la Korea Kaskazini, pamoja na kiuchumi.
Viongozi hao vile vile wamejadiliana kuhusu changamoto za kiuchumi wanazokabiliana nazo kutokana na hatua kali za kibiashara zinazowekwa na jamhuri ya watu wa China kwa maslahi yake.