Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 07:32

Biden alitaka Bunge kusitisha kwa muda kodi ya mafuta ya petroli


Rais Joe Biden akizungumzia pendekezo lake la kusitisha kwa muda tozo ya kodi ya mafuta ya petroli, White House, June 22, 2022. Picha ya AP

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano ameliomba bunge kusitisha kodi ya serikali kwenye mafuta ya petroli kwa kipindi cha miezi mitatu ili kukabiliana na bei ya juu sana ya mafuta, lakini baadhi ya wabunge kutoka chama chake wamesema huenda ombi lake lisitekelezwe.

Familia za Wamarekani ambazo zinalipa pesa nyingi za mafuta ya petroli zinahitaji afueni ya kifedha, Biden amesema huku akilishinikiza bunge kuchukua hatua, alipoeleza kuwa pendekezo lake la kusitisha kodi ya centi 18.4 kwa galoni moja halitoshi.

“Naelewa sana kwamba kusitisha kwa muda tozo ya kodi ya mafuta pekee haitamaliza tatizo lakini itazipa familia afueni ya haraka, nafuu kidogo, wakati tunaendelea kufanya kazi ili kupunguza bei ya mafuta kwa muda mrefu,” Biden amesema.

Rais ameyataka pia majimbo kusitisha kwa muda tozo ya kodi ya mafuta, ambayo mara nyingi iko juu zaidi kuliko kodi ya serikali kuu.

Ameomba pia kampuni kubwa za mafuta kutoa mapendekezo juu ya jinsi ya kurejesha uwezo wa viwanda vya kusafisha mafuta watakapokutana leo Alhamisi na waziri wa nishati Jennifer Granholm.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG