Akizungumza Jumatano baada ya kuwasili mjini Washington kutoka mjini Glasgow, Scotland, Rais huyu alisema kushindwa huko kunaashiria umuhimu wa chama hicho kuongeza juhudi zake kwa watu wa Marekani, akiongeza kwamba matokeo hayo hata hivyo hayaashirii udhaifu uongozi wake kama rais.
Jimboni Virginia, mdemokrat Terry McAuliffe amepoteza kiti cha gavana kwa mwanasiasa chipukizi mrepablikan Glenn Youngkin katika jimbo ambalo Biden alishinda warepablikan kwa pointi 10 mwaka mmoja uliopita.
"Hakuna mtu amewahi kuchaguliwa kuwa gavana wa Virginia akitoka kwa chama cha Rais aliyeko madarakani," alisema.
Hata hivyo, kauli imekosolewa na shirika la habari la AP, kwa sababu mmoja wa wagombea, Glen McAuliffe aligombea na kushinda wakati wa utawala wa Rais Barack Obama, wote wawili wakiwa Wademokrat.
Alikuwa wa kwanza kufanya hivyo ndani ya kipindi cha miaka 44.
Biden aliongeza kwamba katika nyakati hizi, watu wengi wameghadhabishwa na janga la corona, ukosefu wa ajira pamoja na ongezeko kubwa la bei za mafuta.
Biden aliyasema hayo mbele ya wanahabari katika ikulu hapa Washington, wakati akitangaza hatua ya kuanza kutoa chanjo za covid kwa watoto wa kati ya umri wa miaka 5 hadi 11 hapa Marekani, akisema ni hatua kubwa kwenye vita dhidi ya janga hilo.
Kukosa kwake kulishawishi bunge kuidhinisha dola trilioni 1 za kukarabati miundombinu pamoja na mwingine wa dola trilioni 1.75 za kufadhili program za kijamii na hali ya hewa kabla ya uchaguzi huo haukuonekana kuleta taofauti yoyote, kwa mujibu wa shirika hilo la habari.