Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:21

Biden ahimiza kuidhinishwa kwa mswaada wa haki za upigaji kura


Rais wa Marekani Joe Biden akieleza hatua za kulinda haki ya kupiga kura katika hotuba yake kwenye Kituo cha Taifa cha Katiba,aiPhiladelphia, Pennsylvania, July 13, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden akieleza hatua za kulinda haki ya kupiga kura katika hotuba yake kwenye Kituo cha Taifa cha Katiba,aiPhiladelphia, Pennsylvania, July 13, 2021.

Rais Joe Biden wa Marekani alikuwa mjini Philadelphia, Jumanne, usiku, kuhimiza kuidhinishwa kwa mswaada wa sheria kuhusu haki za upigaji kura ambao umekwama bungeni.

Alichukuwa hatua hiyo wakati mabunge ya majimbo yanayodhibitiwa na Warepublikan wanapitisha sheria kubana masharti ya upigaji kura kwenye majimbo yao.

Hata hivyo Rais Biden hakufafanua namna ya kupambana na juhudi hizo za Warepubican.

Philadelphia ambayo iko katika jimbo la Pennsylvania ndiko kulikozaliwa demokrasia ya Marekani, mji wenye kengele ya uhuru inayo mulika mahala tangazo la uhuru lilikotolewa.

Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Na hapo ndipo Rais Biden alitoa hotuba yake jana akifufua juhudi zake za kulinda haki za upigaji kura.

Rais Biden alieleza : "Tunawaomba marafiki zetu Warepublikan kwenye bunge na na majimbo, wilaya na miji kusimama, kwa hisani zenu na kusaidia kuzuia juhudi hii ya dhati ya kuhujumu mfumo wetu wa uchaguzi na haki ya msingi ya kupiga kura. Hamna haya?"

Biden alitoa wito kwa Wademokrat kuungana na kupigania hilo. Lakini hakufafanua mkamati mpya wa kusukuma mbele mswaada wa sheria ya kitaifa ambayo intapanua uwezo wa watu kupiga kura. Hata hivyo mswaada huo ulipingwa na Warepublican mwezi wa Juni.

Hapa Marekani serikali za majimbo na wala sio serikali kuu ndio huamua jinsi Wamarekani wanavyoweza kupiga kura na vipi kura zinahesabiwa. Mwaka huu karibu majimbo 17 kati ya 50 yenye Warepublikan wengi kwenye mabunge hayo wamepitisha sheria ambazo Wademokrat wanasema zinafanya hali kuwa ngumu kwa watu kupiga kura hasa wale wachache na Wamarekani weusi.

Jimbo moja ambalo liko katika mchakato wa kubadili sheria zake ni Texas ambapo hapo Jumatatu wabunge wa chama cha Demokrat waliondoka bungeni na kuelekea Washington wakati wa kujadili mswaada wa upigaji kura. Ikiwa ni hatua ya kuzuia utaratibu kuendelea bila ya akidi inayohitajika.

Bunge la Texas
Bunge la Texas

Chris Turner ni mbunge wa chama cha Demokrat kutoka jimbo la Texas.

Turner alikuwa na haya yakusema : "Juhudi za kitaifa za warepublican kubana upigaji kura, juhudi dhidi ya wapiga kura zina fikia kiwango cha mzozo katika jimbo la texas hivi sasa.

Warepublican wanadai sheria zinapangwa kuondowa ubadhirifu katika uchaguzi.

John Comyn Seneta wa Marekani : "Ni upotoshaji na sio kweli kabisa kudai kwamba juhudi zezote za kuzuia ubadhirifu ni sawa na juhudi za kubana upigaji kura."

Haki ya upigaji kura imekuwa kiini cha mvutano wa kisiasa hapa Marekani. David Schultz wa Chuo Kikuu cha Minnesota anasema mvutano unatokana na madai ya Rais wa zamani Donald Trump kwamba aliibiwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.

Schultz anafafanua kwa kusema : Kile kinacho sababisha hali hii ni hasa madai ya Donald Trump tangu mwaka 2016 aliposema ikiwa hatashinda kwenye uchaguzi itakuwa ni kwa sababu ya wizi wa kura. Ametoa madai hayo hayo kabla ya uchaguzi wa 2020 na baadaye. Na wafuasi wake WarepubliKan kufikia hapa wamependa hoja yake hiyo.

Na hapo jana Rais Biden alikemea kabisa hoja hiyo akisema ni uongo mtupu. Hauna msingi wowote.

Vyanzo vya habari : AFP / AP

XS
SM
MD
LG