Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 09, 2023 Local time: 05:29

Biden afanya kikao na kiongozi wa Palestina


Rais wa Marekani Joe Biden na rais wa Palestina Mahmoud Abbas mapema Ijumaa.

Rais wa Marekani Joe Biden ambaye yuko katika ziara ya mashariki ya kati Ijumaa amekutana na kiongozi wa Palestina Mahmud Abbas.

Viongozi hao wamekutana huko ukingo wa magharibi, kwa mazungumzo yaliojikita zaidi kwenye maendeleo ya kiuchumi ukiwemo ufadhili wa hospitali mashariki mwa Jerusalem. Biden ametangaza msaada wa dola milioni 100 kwa ajili ya taasisi za afya kwenye eneo hilo ikiwa sehemu ya ahadi ya miaka kadhaa kutoka kwa Marekani.

Mazungumzo hayo pia yameangazia ushirikiano wa kiuchumi katika kuimarisha huduma ya mawasiliano ya 4G kwenye eneo la Gaza na Ukingo wa magharibi. Baadaya ziara yake katika eneo la Palestina Biden ameelekea Saudi Arabia ambako tangazo lilifanyika Alhamisi la kufungua safari za ndege za kimataifa ikiwa na maana kwamba ndege za Israel sasa zinaweza kuingia nchini humo.

Alhamisi Biden alifanya mazungumzo na waziri mkuu wa muda wa Israel Yair Lapid, ambapo baadaye walihutubia wanahabari na kusema kwamba wamekubaliana kutoruhusu Iran kutengeneza silaha za nyuklia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG