Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 06:16

Biden aahidi msaada kwa watu walioathirwa na dhoruba Kentucky


Rais wa Marekani Joe Biden akiwa kwenye mji wa Dawson Springs, Kentucky

Rais wa Marekani Jumatano ametembelea jimbo la Kentucky ili kujionea mwenyewe hasara iliyosababishwa na vimbunga kadhaa vya nguvu sana na  kuacha takriban watu 74  wamekufa huku maelfu wengine wakiwa hawana makazi mwishoni mwa juma. 

Ijumaa na Jumamosi liyopita, Biden aliarifiwa kuhusu hali ilivyokuwa kuhusu juhudi za uokozi kutoka na dhoruba ambayo ilipiga vibaya jimbo la Kentucky na majimbo jirani. Alitembea kwa helikopta majimbo yaliyokumbwa na dhoruba ambako alishuhudia majengo yalioporomoka pamoja na manusura waliokuwa wakitembea barabarani.

Kiongozi huyo wakati wa ziara ya Jumatano ameahidi msaada kutoka serikali kuu akisema kwamba kutokana na uharibifu uliotokea, baadhi ya miji italazimika kujengwa upya. Gavana wa jimbo la Kentucky Andy Beshear amesema Jumanne kwamba zaidi ya watu 100 hawajulikani walipo jimboni humo na hasa kwenye mji mdogo wa Dawson Springs wenye takriban 3,000.

Msemaji wa ikulu ya Marekani Karine Jean Pierre aliwaambia wanahabari waliokuwa ndani ya ndege ya rais kwamba ujumbe wa rais ulikuwa wa kuwahakikishia watu walioathirika kwamba serikali yake itafanya kila iwezalo kuhakikisha wamerudi kwenye hali ya kawaida ya maisha.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG