Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 15:00

Bibi wa miaka 104 apona mara ya pili kutokana na COVID-19


Bibi wa miaka 104 apona mara ya pili kutokana na COVID-19
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:40 0:00

Madaktari wakimpongeza bibi mwenye umri wa miaka 104 aliyepona baada ya kuuugua mara ya pili COVID-19

Bibi huyu ni kutoka kaskazini mwa nchi ya Colombia amepona kutokana na virusi vya Corona kwa mara ya pili, kwa mujibu wa madaktari wa eneo analoishi, baada ya kuruhusiwa Jumatatu, Aprili 5, 2021. Carmen Hermandez alilazwa hospitali kwa siku 21 akipigania maisha yake.

Hernandez, anatokea Tunja, kilomita 119 kaskazini mwa mji mkuu wa Colombia, aligunduliwa ana COVID-19 kwa mara ya kwanza mwezi Juni, 2020 na kutibiwa katika nyumba ya kuwalea watu wazima ambako ameishi kwa miaka 25.

Hernandez alipokea dozi ya kwanza ya chanjo ya Sinovac Februari 26, kabla ya kugunduliwa ana COVID-19 kwa mara ya pili Machi 8. Kipimo cha hivi karibuni kinacho onyesha ana COVID-19 ilipelekea kucheleweshwa kupewa dozi ya pili ya chanjo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG