Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 11:36

Biashara ya madini DRC yakumbwa na wasi wasi


Watu wanachekecha mchanga kupata almasi katika machimbo ya Kabuebue katika kijiji cha Bakua Bowa karibu na Mbuji-Mayi nchini Congo.
Watu wanachekecha mchanga kupata almasi katika machimbo ya Kabuebue katika kijiji cha Bakua Bowa karibu na Mbuji-Mayi nchini Congo.

Serikali za Kivu ya Kaskazini na Kusini huko DRC na wanaharakati na wafanyabiashra wataka muda zaidi kabla ya kuanza kuidhinishwa madini yanayosafirishwa Marekani.

Kuanzia tarehe mosi April 2011, makampuni ya Marekani hayataweza kununuwa madini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bila ya kuidhinishwa kwamba yametokea maeneo ya usalama.

Hatua hii inatokana na kanuni ya bunge la Marekani na kutiwa saini na Rais Barack Obama inayohitaji makapuni ya Marekani kuhakikisha yananunua madini kutoka wafanyabishara wasio husika na mapigano au maeneo yasiyoshikiliwa na waasi huko DRC.

Akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka Goma, mwanasheria Athumani Mpina anasema tatizo hilo linatokana na ukweli kwamba serikali ya Kinshasa haikufanya lolote katika kutayarisha utaratibu wa kukagua na kuidhinisha madini ya nchi hiyo.

"Kwa kipindi cha miezi sita serikali ilipiga marufuku uchimbaji wa madini huko mashariki ya nchi lakini haikuchukuawa hatua zozote kupanga sheria au kanuni kuhusiana na uchimbaji madini kwa njia ya haki katika kipindi hicho", alisema Bw Mpina.

Wanaharakati, wafanyabiashara na wachimbaji madini wa Kongo wanaitaka serikali ya Kinshasa kuiomba Washington kuongeza muda kwa angalau miezi sita ili serikali ipange utaratibu wa ukaguzi.

XS
SM
MD
LG