Mwanamuziki Beyonce Knowles hatimaye alipata tuzo ya albamu bora kwa rekodi yake ya muziki wa Country iitwayo 'Cowboy Carter' ambayo pia alishinda albamu bora ya muziki huo, tuzo ambayo alionekana kushtushwa kuipokea huko Los Angeles California katika usiku wa Tuzo za Grammy siku ya Jumapili.
Ni ushindi mkubwa baada ya kushindwa mara kadhaa hapo awali katika kuwania Albamu Bora ya Mwaka na Beyonce sasa akikusanya Grammys za maisha kuliko msanii mwingine yeyote.
Sherehe za Grammy za mwaka huu zilifanyiwa marekebisho na kuwa sehemu ya onyesho la tuzo na sehemu ya kuchangisha fedha kwa watu walioathiriwa na moto hivi karibuni katika eneo la Los Angeles, ambao uliuwa watu 29 na kuwafanya maelfu ya watu wakiwemo wanamuziki wengi kuyahama makazi yao.
Mtangazaji Trevor Noah aliwaelekeza watazamaji wakati wa matangazo hayo katika kuchangia fedha.
Wakati fulani Noah alisema takriban dola milioni 7 zilikusanywa usiku huo.
Kuhusu tuzo hizo, Kendrick Lamar alikuwa mshindi mwingine mkubwa katika usiku huo.
Rapa huyo alishinda rekodi ya mwaka na wimbo bora wa mwaka wa "Not Like Us," katika wimbo wa ugomvi wake na rapa wa Canada Drake.
Forum