Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 07:00

Besigye aachiliwa kwa dhamana


Kiza Besigye akizuingumza na waandishi habari baada ya kuachiliwa kwa dhamana.

Mahakama kuu ya Uganda, siku ya Jumanne ilimuachilia kwa dhamana kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye, ambaye amekuwa kizuizini tangu mwezi Mei.

Jaji Wilson Masalu Musene alimamrisha Besigye kuachiliwa kwa dhamana ya dola 30,000 za Marekani.

Aidha jaji huyo alimwamuru Dkt Besigye, ambaye ndiye kiongozi wa chama cha Forum for Democratic Change (FDC) kutojihusisha na vitendo vya kuzua ghasia. Ame mtaka Besigye adumishe amani katika jamii hadi kesi ya uhaini inayomkabili itakaposikizwa na uamuzi kutolewa.

Besigye aliwekwa rumande mwezi Mei baada ya kukamtwa kwa tuhuma za uhaini, kufuatia video ilyochapishwa kwenye tovuti ya Youtube, iliyomuonyesha akiapishwa kama rais wa Uganda baada ya uchaguzi mkuu wa mweziu Februari mwaka huu.

Mahakama hiyo pia imemtaka Besigye awe akifika kortini mara moja kila wiki mbili kuanzia Julai 26. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, Besigye amerejeshwa seli kusubiri kukamilishwa kwa utaratibu wa kumwachilia huru kwa dhamana hiyo.

Besigye amekuwa mpinzani mkali kwa rais Museveni na amezuiliwa mara nyingi nyumbani kwake na kwenye vituo vya polisi kabkla ya kufunguliwa mashtaka yanayomkabili kwa sasa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG