Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 14:22

Besigye: Kushiriki uchaguzi Uganda ni kupoteza wakati


Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Dkt Kizza Besigye

Akiwa kwenye ziara ya siku mbili nchini Kenya, kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Dkt Kizza Besigye, alisisitiza kauli yake ya awali kwamba utawala wa rais wa taifa hilo, Yoweri Kaguta Museveni, unaendelea kuwakandamiza wananchi wake.

Besigye, ambaye alizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika siku ya Jumanne katika mahojiano ya kipekee jijini Nairobi, alisema kuwa haupo umuhimu wowote kwa raia wa Uganda kushiriki uchaguzi "ambao unafanyiwa ukarabati na wandani wa Museveni."

Na kutokana na hayo, mwanasiasa huyo alisema ni sharti sasa raia wa Uganda wahimize mabadiliko muhimu katika taasisi muhimu nchini humo. La sivyo wataendelea kutekwa nyara na kiongozi huyo ambaye amekaa madarakani zaidi ya miaka thelathini.

Mwandishi wa VOA mjini Nairobi, Kennedy Wandera, alizungumza na kiongozi huyo na kuanza kwa kumuuliza msimamo wake kuhusu hatua za wabunge kuondoa kizuizi cha ukomo wa umri kwa mgombea wa urais ili kushiriki uchaguzi. Sikiliza:

please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:03:12 0:00

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG