Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 16:04

Bernie Sanders awashutumu viongozi wa Democrat


Mgombea urais wa Democrat, Seneta Bernie Sanders. May 8, 2016.
Mgombea urais wa Democrat, Seneta Bernie Sanders. May 8, 2016.

Mgombea urais wa Marekani, Bernie Sanders amezidisha mapambano yake na viongozi wa chama cha Democratic kwa kumuunga mkono mkuu wa Democratic National Committee - DNC na kuwashutumu kwa kujaribu kumpendelea mpinzani wake Hillary Clinton kama mgombea wake wa urais.

Katika mifululizo ya mahojiano ya televisheni Jumapili, Sanders alikiri kwamba yupo katika mapambano makali ya kumpita Clinton, mgombea anayeongoza. Pia alisema kwamba kama anashinda kuingia White House hatomteuwa tena Debbie Wasserman Schultz kama mwenyekiti wa DNC. Badala yake alimuidhinisha profesa wa sharia, Tim Canova ambaye anampa changamoto mbunge huyo mwanamke wa jimbo la Florida katika uchaguzi wa awali wa Democrat katika jimbo hilo mwezi Agosti.

Mwenyekiti wa DNC, Debbie Wasserman Schultz.
Mwenyekiti wa DNC, Debbie Wasserman Schultz.

Wasserman alitoa taarifa akisema ataendelea kutoegemea upande wowote katika kinyang’anyiro cha urais kwa Democrat licha ya matamshi kutoka kwa Sanders. Clinton alisema kwamba tayari anajihesabu yeye kuwa ni mteuliwa wa chama na anaelekeza mapambano yake kwa Donald Trump mgombea anayeonekana kupata uteuzi wa chama cha Republican.

Clinton anamuita Trump ni hatari. Kwa mujibu wa uchunguzi wa kura ya maoni hivi karibuni Clinton na Trump wapo kwenye kinyang’anyiro kikali na wapiga kura wengi wakiwaangalia wote siyo chaguo lao.

Uchunguzi mmoja wa kura ya maoni uliotolewa Jumapili na The Washington Post-ABC News ulionesha kwamba Trump akiwa nyuma kiasi wakati kwenye maoni ya kituo cha televisheni cha NBC na Wall Street Journal yalionesha Clinton akiwa anaongoza kiasi.

XS
SM
MD
LG