Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 16:24

Bernie Sanders asema hatojitoa kinyang'anyiro cha urais cha Democrat


Mgombea urais wa Democrat, Hillary Clinton akizungumza na wafuasi wake huko Louisville, Kentucky.
Mgombea urais wa Democrat, Hillary Clinton akizungumza na wafuasi wake huko Louisville, Kentucky.

Kampeni za kisiasa nchini Marekani zinaangaliwa na baadhi ya watu kwa mtazamo tofauti kwa upanda wa chama cha Democrat kufuatia ushindi wa Jumanne wa seneta wa Vermont, Bernie Sanders aliyepata asilimia 51 dhidi ya mpinzani wake waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton aliyepata asilimia 36 katika uchaguzi wa awali kwenye jimbo la West Virginia.

Bwana Sanders aliwaambia wafuasi wake kwamba ataendelea kupambana katika kinyang’anyiro hiki cha kuwania uteuzi wa chama bila kukata tamaa.

Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa George Kakoti kutoka chuo kikuu cha Nova kilichopo SouthEastern katika jimbo la Florida na alieleza mtazamo wake kwamba kimsingi Sanders hawezi kufikia kura alizonazo Hillary kwa sasa lakini nia ya Sanders kuendelea kuwepo katika kinyang’anyiro cha kuwania uteuzi wa chama ni kuwa na ushawishi katika ilani ya uchaguzi wa chama chake cha Democrat.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:07 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mgombea urais wa Republican, Donald Trump alipokuwa West Virginia
Mgombea urais wa Republican, Donald Trump alipokuwa West Virginia

Wakati huo huo mgombea pekee aliyebaki kwenye kinyang’anyiro cha urais kwa chama cha Republican, Donald Trump anatarajiwa kukutana na viongozi wa juu wa chama hicho siku ya Alhamis huko White House akiwemo spika wa bunge, Paul Ryan ambaye ni mmoja wa baadhi ya viongozi wa chama hicho waliokataa kumuidhinisha Trump katika kampeni hizi za kisiasa zinazoendelea.

XS
SM
MD
LG