Bei za bidhaa zimeongezeka kutokana na kupanda kwa gharama za mafuta na chakula, ambazo serikali ya Rais Yoweri Museveni imedai ni kutokana na athari zinazoendelea za janga la COVID-19 na vita nchini Ukraine. Mfumuko wa bei wa kila mwaka ulifikia 7.9% mwezi Julai kutoka 6.8% mwezi Juni.
"Uchumi unaendelea kukabiliwa na shinikizo kubwa la mfumuko wa bei kutokana na mazingira ya nje, hali ya hewa na kushuka kwa kiwango cha ubadilishaji huku kukiwa na mahitaji duni ya ndani," Naibu Gavana Michael Atingi-Ego aliuambia mkutano wa wanahabari. Benki ilishusha makadirio ya ukuaji wa uchumi wa mwaka huu kutoka asili mia 2.5% hadi 3%, kutoka utabiri wa awali wa 4.5% hadi 5%, ukiakisi gharama za juu za uzalishaji zinazohusishwa na mafuta na usafirishaji.