Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 19:14

Benki ya Dunia yatoa msaada wa dola milioni 300 kwa Msumbiji


Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi

Benki ya dunia Jumatatu imetoa msaada wa dola milioni 300 kwa Msumbiji, kuashiria kurejea kwake nchini humo miaka sita baada ya kusitisha msaada wake wa kifedha kufuatia kashfa ya deni iliyofichwa.

Waziri wa fedha wa Msumbiji Max Tonela amesema pesa hizo zitatumiwa kufadhili miradi ya miundombinu ili kusaidia kuimarisha uchumi na kuboresha hali ya maisha katika nchi hiyo.

“Hii ni bajeti ya kwanza ya msaada wa uhadfili ambayo tunatumai kuiona katika miaka mitatu ijayo,” Tonela amesema kwenye hafla ya utiaji saini katika mji mkuu, Maputo.

Makubaliano hayo yanafuatia mkataba wa dola milioni 456 na shirika la kimataifa la fedha (IMF) uliosainiwa mwezi Mei ulioashiria kuwa Msumbiji imerudi kuaminiwa na wafadhili baada ya kashfa ambayo ilisababisha mzozo mbaya wa kiuchumi tangu taifa hilo lijipatie uhuru kutoka kwa Ureno zaidi ya miongo minne iliyopita.

Serikali ilichukua mikopo ya siri yenye thamani ya dola bilioni 2 mwaka wa 2013 na 2014 kutoka kwa benki za kimataifa ili kununua meli za uvuvi na meli za ukaguzi.

​
XS
SM
MD
LG