Benki kuu ya Libya yenye makao yake mjini Tripoli imesema leo Jumapili itafunga shughuli zote na haitaanza kazi hadi afisa mwandamizi wa benki hiyo aliyetekwa nyara mapema leo atakapoachiliwa.
Benki Kuu ni taasisi pekee inayotambuliwa kimataifa kwa mapato ya mafuta ya Libya, mapato muhimu ya uchumi kwa nchi hiyo iliyogawanyika kwa miaka mingi kati ya serikali mbili hasiju huko mjini Tripoli na Benghazi. Benki hiyo imesema kundi lisilojulikana lilihusika na utekaji nyara leo Jumapili wa Musaab Muslam, mkuu wa idara ya teknolojia ya habari.
“Benki hiyo inapinga mbinu kama vile za kibabe ambazo zinafanywa na baadhi ya makundi nje ya sheria,” ilisema taarifa hiyo. iliongeza kuwa maafisa wengine wa benki hiyo pia wametishiwa na hivyo watasimamisha shughuli hadi zoezi hili litaktabia hizi zitakaposita na mamlaka zinazohusika kuingilia kati.
Forum