Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:02

Benki za India zakabiliwa na upungufu wa fedha taslimu


Muuza duka mmoja wa kihindi akiangalia kwa makini rupia 500 kama ni fedha halali.
Muuza duka mmoja wa kihindi akiangalia kwa makini rupia 500 kama ni fedha halali.

Kutokana na athaqri hii makampuni mengi yamekuwa yakipunguza wafanyakazi kutokana na kuyumba kwa biashara na hivyo viwanda kupunguza wafanyakazi ili kupunguza uzalishaji.

Wafanyakazi nchini India hivi karibuni waliendelea kupanga mstari mirefu nje ya benki moja, Magharibi mwa India kufungua akaunti. Mstari huo ulikuwepo katika ukomo wa barabara katikati ya mji wa Gurgaon, katika jimbo la Haryana.

Mmoja ya wafanyakazi hao Ishwari Lal, ambaye ni kibarua anayelipwa kwa siku. Yeye ni miongoni mwa mamilioni ya wahamiaji kutoka sehemu mbali mbali za India.

Wafanyakazi hawa ni waajiriwa katika viwanda vidogo vidogo au biashara, katika miradi ya ujenzi wa majumba, au ulinzi, udereva, uhudumu.

Muuza vitunguu nchini India akihesabu fedha.
Muuza vitunguu nchini India akihesabu fedha.

Lal siku zote alikuwa analipwa pesa taslimu na kuzitumia kwa uangalifu. Pia hutuma kiwango kidogo cha kipato hicho kwa familia yake. Kiasi kinachosalia anakitenga kwa ajili ya kulipa kodi ya chumba na kununua chakula na mahitaji mbali mbali.

Lakini Lal amelipwa robo ya ujira wake tangu kuzuka tatizo la upungufu wa pesa taslimu lilipoanza ambalo limeiathiri nchi hiyo.

Wiki sita zilizopita, Serikali ya India ilipiga marufuku sarafu ya noti ya thamani ya juu ya rupia 500 ($7.50) na rupia 1,000. Hatua hiyo imelenga kutafuta na kukamata kiwango kikubwa cha fedha chafu zilizoko mitaani.

Mwajiri wake Lal amemtaka afungue akaunti benki ilikupokea mshahara wake. Hivi sasa anafanya hilo japokuwa kuna wasiwasi kwamba itamwiya vigumu kupata pesa zake mara moja atakapozihitaji kutoka benki.

Benki zinakabiliwa na upungufu wa fedha

Tangu serikali ilipopiga marufuku noti hizo mbili, wananchi wengi wamekuwa wanapanga foleni katika mabenki kutoa pesa zao. Na mabenki hawawapi wateja kiwango wanachokitaka kwani wao pia hawana pesa za kutosha kutokana na kucheleweshwa kutumwa pesa kufidia kile kilichotumiwa kuwalipa wateja wao.

“Ikiwa nahitaji rupia 10,000, naweza kuchukua benki rupia 2,000 tu. Vipi nitaweza kuendesha maisha kwa kiwango hiki kidogo? Kwa kweli nimekuwa nikikabiliwa na matatizo mengi,” alisema Lal.

Anajiuliza vipi ataweza kununua chakula, kulipia matibabu na kutuma fedha nyumbani kwa ajili ya watoto wake. Baadhi ya waajiri pia wanakabiliwa na upungufu wa pesa na wameanza kutoa cheki katika malipo ya mishahara.

India ina mamia ya wafanyakazi ambao wameajiriwa katika sekta isiyo rasmi ambao wamelazimika kufungua akaunti benki. Sekta hii ni sehemu ya uchumi ambao hautozwi kodi na wala kudhibitiwa na serikali.

Inakadiriwa kuwa takriban wananchi wa India milioni 48 katika sekta isiyo rasmi wanapokea ujira wao katika fedha taslimu. Hiyo inawakilisha asilimia 80 ya nguvu kazi nchini humo.

Kadiri upungufu wa fedha unavyoendelea, sekta isiyo rasmi inapunguza kasi ya biashara. Hili linaathiri ukuaji wa uchumi katika uchumi mojawapo wa dunia unao ongezeka kwa kasi.

Kutokana na athari hii makampuni yamekuwa yakipunguza wafanyakazi kutokana na kuyumba kwa biashara na viwanda kuwaondoa wafanyakazi kwa sababu ya kupungua uzalishaji.

XS
SM
MD
LG