Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:43

Benjamin Netanyahu kuhutubia Bunge la Marekani


Benjamini Netanyahu akihutubia moja ya mikutano yake kabla ya hotuba yake ya Jumanne. Hii ilikuwa siku ya Jumatatu, Machi 2, 2015, nchini Marekani.
Benjamini Netanyahu akihutubia moja ya mikutano yake kabla ya hotuba yake ya Jumanne. Hii ilikuwa siku ya Jumatatu, Machi 2, 2015, nchini Marekani.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, atalihutubia Bunge la Marekani Jumanne katika hotuba inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

Awali, Netanyahu alisema Marekani, na Israel, zinakubaliana kwamba kuna haja ya kuizuia Iran kuwa na silaha za nyuklia lakini hazikubaliani namna ya kufikia lengo hilo.

Kauli hiyo ilitolewa siku moja kabla ya waziri mkuu huyo kuhutubia bunge la Marekani.

Mwaliko wa kulihutubiua Bunge umezusha utata Marekani kwa sababu unafanyika bila ya utamaduni wa kawaida wa kushauriana na White House.

Hatua hiyo imeonyesha mvutano wa uhusiano uliopo baina ya bwana Netanyahu, na rais wa Marekani, Barack Obama.

Bwana Netanyahu anasema kutokukubaliana na Marekani, kunatokana na mitazamo tofauti kwa sababu Washington, inawasiwasi na usalama wakati Israel inahofu na uhai.

Katika mahojiano na shirika la habarfi la Reuters, bwana Obama amesema utawala wake na serikali ya Israel unatofautiana kwa namna ya kuiwezesha Iran kutokuwa na nguvu za nyuklia.

XS
SM
MD
LG